Baadhi ya waafrika kutokanyaga Marekani Trump akiwa rais?

0
149

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump ametoa hotuba ya kufunga kongamano na kukubali kuteuliwa na chama chake kuwania nafasi hiyo amesema kuwa atasimamisha uhamiaji wa raia kutoka kwenye baadhi ya nchi za Afrika.

Donald Trump aliyetoa hotuba kwa dakika 75 alizungumzia mambo mbalimbali miongoni mwa hayo akazungumzia uhusiano wa Marekani na Afrika endapo atachaguliwa kuwa rais.

Alimkosoa aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambaye pia ni mpinzani wake Hillary Clinton kuwa katika kipindi cha uongozi wake nchi kadhaa za Afrika ziliingia kwenye machafuko makubwa na kupelela kuzaliwa kwa makundi ya kigaidi.

‘Mwaka 2009, kabla ya uongozi wa Hillary, kundi la Isis halikuwepo hata kwenye ramani. Libya ilikuwa imara. Misri ilikuwa na amani’

Mwisho na muhimu zaidi, ni lazima tusitishe uhamiaji mara moja kutoka kwenye nchi ambazo zimekumbwa na athari ya ugaidi mpaka utakapofika wakati ambapo namna bora ya kuwachuja itakapokuwa imepatikana. Hatuwataki kwenye nchi yetu.

Nchi zinazoweza kukumbwa na athari ya watu wake kuzuiwa kuingia Marekani iwapo kauli hii itatekelezwa ni pamoja na Nigeria, Kenya, Cameroon, Somalia), Libya, Tunisia na Mali.

LEAVE A REPLY