Baada ya kutendwa na mkewe, Nuh Mziwanda aondoa wazo la kuoa

0
391

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amesema kuwa kwasasa hataki kabisa suala la kuoa na kusikia suala la mapenzi baada ya kuachana na mke wake.

Nuh Mziwanda ambaye siku za hivi karibuni aliachana na aliyekuwa mke wake Nawal amesema kuwa kwasasa anajielekeza zaidi katika kazi na si masuala ya mapenzi.

Alipoulizwa iwapo ana mipango ya kuja kuoa siku za mbeleni baada ya hivi karibauni ndoa yake kuvunjiaka alisema itatengemea kwa sababu yeye ni binadamu pia.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Pia mimi ni mtoto wa kiume na ndoa ni jambo jema kwa hiyo siwezi kusema sitakuja kuoa kwa sababu huwezi kujua nini kitatokea mbele yangu,”.

Nuh Mziwanda ambaye ana historia ya kuwa katika mahusiano na msanii Shilole mwaka huu ameachana na aliyekuwa mke wake wa ndoa ambaye pia walijaliwa kupata mtoto mmoja.

LEAVE A REPLY