Baada ya kuitosa RockStar4000, Jide apata uongozi mpya

0
107

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amepata uongozi mpya ambao utasimamia kazi zake za muziki baada ya kuachana na lebo ya RockStar400.

Mwanamuziki huyo kwasasa amepata uongozi huo mpya wa kampuni kutoka Nigeria ambao wanafanya kazi nchini Kenya.

Kampuni hiyo inafahamika kama Taurus Muzik ambayo pia inafanya kazi na wasanii kama Dela Maranga na Kagwe Mungai na Urban Hype kutoka Zambia.

Jaydee ameshaanza kufanya kazi na kampuni hiyo na watatoa taarifa rasmi hapo baadae. Jide atatarajiwa kuwa na ziara ya muziki nchini Afrika Kusini mwezi Disemba mwaka huu.

Mwanamuziki huyo kabla ya kujinga na lebo hiyo alikuwa chini ya lebo ya RockStar4000 inayomilika na Seven Mosha ambapo pia inammiliki Alikba.

LEAVE A REPLY