Azam FC yakaribia kumsajili mshambuliaji wa Medeama

0
188
Enock Atia Agyei of Medeama SC during the CAF Confederation Cup between Medeama SC and Young Africans 26 july 2016 playing in Sekondi Ghana © Christian Thompson/BackpagePix

Klabu ya Azam FC imefikia makubaliano na Medeama FC ya Ghana kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Enoch Atta Agyei.

Mtendaji mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba yupo Ghana kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na taarifa zinasema ametekeleza jukumu hilo vizuri.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Windy Professionals aliivutia Azam FC akiichezea Medeama wiki tatu zilizopita jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

Kinda huyo wa miaka 17, alifunga mabao 17 katika Ligi Daraja la Kwanza ya GN Bank akiwa na Windy Professionals kabla ya kuhamia Medeama FC .

LEAVE A REPLY