AY athibitisha kumiliki nyumba nchini Marekani

0
578

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya maarufu kama AY amethibitisha kumiliki mjengo wa kifahari nchini Marekani katika maeneo ya Calabasas.

AY  amethibitisha kwamba akili yake inafikiri mbali zaidi na yeye ni wa anga za kimataifa, naye aka­nunua Mjengo maeneo ya Calabasas ingawa hajataka kufafanua gharama zake.

AY anakuwa Kama ametisha hivi kwani eneo ambalo amenunua mjengo wake ni eneo wanalokaa washua na mastaa wakubwa wenye pesa zao Kama vile Kim Kardashian, Kanye West, Drake, Justin Bieber na wengineo wengi.

Mwanamuziki huyo anakuwa mwanamuziki wa kwanza kutokea Tanzania kumiliki nyumba katika eneo hilo la Calabasas nchini Marekani.

LEAVE A REPLY