AY afunguka mipango yake ya mwakani

0
129

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ ametoa ahadi kwa mashabiki wake kuwa mwaka 2019 atakuwa msanii wa tofauti  kwa kutoa ngoma mfululizo.

AY amesema kwamba anaamini yeye ana uwezo mkubwa kiasi kwamba hata akiachia wimbo kwa muda wa miaka miwili bado utaishi na kupigwa mara kwa mara na hata  kwenye kumbi za starehe nyimbo zake za mwaka 2013 na bado zinafanya vizuri mpaka sasa.

“Natumaini mwaka 2019 mashabiki zangu wataniona kila sehemu na sio kwamba natoa tahadhari kwa mtu yeyote lakini nasema tu nataka kurudi, na nina mpango wa kufanya kazi na wasanii wengi akiwemo Mwana Fa na Fid Q kwa kuwa ni watu ambao sijafanya nao kazi kwa mda mrefu kidogo hivyo naamini kazi zitakazokuja zitawafurahisha mashabiki zetu,”.

AY pia amesema anafurahishwa na mwenendo wa muziki wa Bongo Fleva vile ambavyo umekuwa ukikua siku hadi siku na kusema kwamba lebo yake ya ‘Unit Entertainment’ ipo ila inafanya maswala ya matangazo na vipindi zaidi, ambapo sasa amesimama kusimamia wasanii kwa kuwa wasanii wa Bongo ni pasua kichwa.

 

LEAVE A REPLY