Aunty Ezekiel: Maadili machafu ya wasanii wamechangia kushuka kwa Bongo Movie

0
350

Muigizaji nyota wa Bongo movie, Aunt Ezekel amesema kuwa sababu iliyochangia kushuka kwa soko la filamu nchini ni matendo machafu ya wasanii wa tasnia hiyo nchini.

Aunty Ezekiel ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyeza na Mose Iyobo amedai wasanii wengi wa filamu wameendekeza starehe kuliko kazi.

Aunty amesema kuwa “Kipindi hiki filamu zimepoteza mvuto na watu wamekuwa wakizungumza mengi ila ninachoona mimi ni matendo yetu machafu yanachangia,”

Pia ameongeza kwa kusema “Mbona wasanii kama kina King Majuto bado wanafanya vizuri? Skendo zinayumbisha soko la filamu na siyo kitu kingine,”

Kati ya skendo ambazo zinatajwa zaidi kuwatikisa wasanii wa kike wa filamu ni kutoka na waumume wa watu, kuolewa na kuachika.

Muigizaji huyo kwasasa anatamba na filamu yake mpya inayokwenda jina la Christmas EVa iliyoingia sokoni mwishoni mwa mwaka jana.

LEAVE A REPLY