Aunty Ezekiel ashangazwa na Shamsa Ford

0
33

Muigizaji wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel amesema kuwa msanii mwenzake Shamsa Ford hajitambui ndio maana anaongea mambo ya familia za watu bila kupewa ruhusa.

Aunty amesema kwamba siku zote katika maisha yake hawezi kubishana na mtu ambaye sio mstaarabu kwa sababu na yeye atakuwa hivyo.

Aunty ambaye ni mzani mwenza na dansa wa Diamond,Mose Iyobo amesema kuwa hawezi kujibizana na Shamsa kwa sababu hajitambui, huwezi ukazungumza mambo ya watu tena ya ndani bila ruhusa ya wenyewe.

Pia amesema kuwa mambo yote aliyozungumza Shamsa hana uhakika nayo, namuacha aendelee kuwa msemaji wangu sina muda wa kuhangaika naye.

Shamsa amekuwa akimrushia maneno Aunt mitandaoni akimsema kuhusu suala la kubeba ujauzito ambao mpaka sasa haijulikani baba mtoto wake.

LEAVE A REPLY