Aunty Ezekiel akanusha kufunga Pub yake kisa kudaiwa kodi

0
53

Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za kufungwa pub yake Baada ya kushindwa kulipia kodi.

Kumekuwa na tetesi kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Pub ambayo ilikuwa inamilikiwa na Aunty Ezekiel iliyopo maeneo ya Kinondoni imefungwa kutokana na mwanamama huyo kukosa kodi.

Aunty alisema siyo kwanza amefunga Pub yake kwa sababu ya kudaiwa kodi bali eneo hilo anataka kufanya biashara nyingine na hiyo ya pub ataihamishia sehemu nyingine.

Mbali ya Aunty Ezekiel kumiliki Pub hiyo Lakini pia anamiliki sabuni ya Murua ambazo amesema kuwa zinauzika vizuri sana.

LEAVE A REPLY