Aunty Ezekiel afunguka kupotea kwenye movie

0
96

Muigizaji wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel amesema kuwa mastaa wengi wameanza kusahaulika katika jamii kutokana na kuhangaika na maisha kuliko ilivyokuwa zamani.

Kauli ya muigizaji imekuja baada ya hivi karibuni kutoonekana kwenye kazi yake ya uigizaji mpaka kupelekea mashabiki wake kumuuliza kinachoendelea.

Aunt alisema kasi ya maisha ya sasa inafanya kila mtu apambane na hali yake na kupunguza baadhi ya mambo waliyoyazoea.

“Hatuonekani mara kwa mara, wala kusikika siku hizi kwa sababu maisha yamekuwa magumu, ni lazima kujituma zaidi na sio kujionesha au kuubeba umaarufu tu huku maisha yako yanateketea,”.

Aunty ni mingoni mwa waigizaji bora sana hapa nchini kutokana na ubora wa kazi zake za filamu mbele ya mashabiki wake.

LEAVE A REPLY