Aunt Ezekiel akanusha kumfamania Mose Iyobo

0
59

Muigizaji wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel amefunguka na kusema kuwa hana muda mchafu wa kufuatilia mambo ya uzushi katika mitandao baada ya kuzishiwa kumfumania mpenzi wake Mose Iyobo.

Amesema anachokijua ni kwamba, kuna watu wanatafuta kiki mitandaoni kupitia jina lake na ndiyo maana hata huo uzushi wa kupigana anaona ni wa kipuuzi.

“Kuna wakati mtu anakuchokonoa hadi inafika mwisho, ukija kuuliza kulikoni unasikia ni mtu anatafuta kiki isiyokuwa na maana.

“Mimi siwezi kupigana na mtu yeyote,” amesema Aunt anayesemekana kwamba siku hizi anawajibu vibaya hata mashabiki wake kwenye Instagram.

Aunt ameendelea kusema  kuwa, anasikia alipigana na Nancy kwa ajili ya Iyobo, jambo ambalo halijawahi kutokea na hafikirii kufanya hivyo, ingawa kuna watu wanamchokoza.

“Kiukweli mtu akinichokoza nitakula naye sahani moja, lakini ishu ya kusema nimepigana, sitaki kumpa mtu kiki. “Kila mtu atafute njia ya kupata kiki na siyo kupitia migongo ya watu wengine,” amesema Aunt.

Inasemekana, wakati Aunt alipotengana na Iyobo kwa miezi kadhaa mwaka jana, Nancy ndiye aliyechukua nafasi hiyo ya Aunt na baada ya wawili hao kurudiana, ndipo uhasama kamili ukaibuka.

LEAVE A REPLY