Audio: Diamond Platnumz ‘SIMBA’ alivyopiga stori na rais Magufuli kwa simu

1
7190

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekuwa staa wa kwanza wa Bongo Fleva kupigiwa simu moja kwa moja na rais John Magufuli na kupongezwa kwa kazi yake.

Rais Magufuli alitumia fursa ya Diamond Platnumz kualikwa kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV kwaajili ya kumpongeza staa huyo pamoja na wasanii wengine wa muziki na maigizo.

Platnumz anaye aliitumia fursa hiyo kumuomba msaada rais Magufuli kupitia serikali yake kuwasaidia wasanii kuwekewa miundombinu bora ya kutekeleza majukumu yao ili nao waweze kujipatia vipato na kuwasaidia watu wengine wenye vipaji kuweza kujiajiri.

Licha ya kuwa mmoja wa mastaa wenye mafanikio makubwa zaidi Bongo lakini pia Diamond alikuwa mmoja wa wasanii waliotumiwa na CCM wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na walikuwa na ushawishi mkubwa uliochangia rais Magufuli kushinda uchaguzi mkuu.

Sikiliza mazungumzo yao moja kwa moja.

Audio kwa hisani ya mtandao wa @Bongo5

1 COMMENT

LEAVE A REPLY