Audio: Diamond Platnumz ‘anakata tawi alilolikalia?’

0
2974

Mpaka kufikia katikati ya miaka ya 2000 hakukuwa na mshabiki yeyote wa muziki aliyesumbuka kutafuta jina Diamond Platnumz mahali popote pale kwaajili ya kumsikiliza Naseeb Abdul.

Lakini jina Diamond lilianza kusikika na kupata umaarufu kwenye miaka ya mwishoni mwa 2000 kisha ilipoanza ngwe nyingine ya umri wa viumbe hapa duniani ndipo jina Diamond lilipojiimarisha kwa mashabiki wa muziki kupitia msaada mkubwa vyombo vya habari.

Hakuna aliyemjua Diamond wala kumjali sana alipowaburudisha watoto wenye ulemavu kwenye siku maalum iliyoandaliwa na Dkt. Reginald Mengi kisha Diamond kutoa burudani.

Baadae watu wakaanza kuisikia ngoma yake MBAGALA kisha KAMWAMBIE na kisha jina Diamond likaanza kupata umaarufu mkubwa.

Wakati huu Diamond hakutegemea SOCIAL MEDIA (mitandao) alitegemea zaidi kusikika redioni na kuonekana kwenye vituo vya Televisheni LAKINI leo Diamond Platnumz anasema ‘Mwandishi atakayemuandika kwa ubaya anapoteza muda wake?’

Diamond amesahau kuwa alikuwa msanii maarufu kwa kutembea na wasanii wa kike kisha kubwagana baada ya muda mfupi na habari hizo ndizo zilizompa umaarufu zaidi?

Diamond amesahau kuwa wasanii wanaamini ‘bila skendo huwezi kufanikiwa?’

Diamond anasahau kuwa naye ni msanii na kabla ya kupata mafanikio aliyoyapata leo alikuwa na skendo mbalimbali ikiwemo ya kumtelekeza baba yake mzazi? Na ni habari za aina hiyo ndizo zilizokuza jina lake?

Diamond anaposema ‘waandishi wanamuandika vibaya’ anamaanisha nini?

Swali linalokuja ni: ‘anaandikwa vibaya au anaandikwa kwa namna ya ubaya anaoufanya?’

Diamond Platnumz ni kweli pengine wewe ndiye msanii mwenye mafanikio zaidi hapa nchini (kwa upande fulani) lakini hiyo haikupi nafasi ya kusema waandishi wanaokuandika vibaya wanapoteza muda wao…..

Kumbuka vyombo vya habari na taaluma ya habari kwa ujumla wake ni kubwa kuliko wewe na mafanikio yako na ni taaluma hiyo iliyosaidia wewe kufika hapo ulipo.

Utakapokosea ‘kama binadamu’ utakumbushwa ‘bila kujali utajiskiaje’ na utakapofanya vizuri ‘utapongezwa na kuhimizwa kufanya jitihada zaidi’ kama unavyopongezwa na kuhamasishwa.

Ni jambo zuri kuona teknolojia imekua na Platnumz anaitumia vizuri kuhakikisha anawafikia mashabiki wake kwa wepesi zaidi lakini ni hatari kuwazungumzia waandishi wa habari kwa kujenga taswira kwa mashabiki kuwa wao ‘waandishi’ wana lengo la kumporomosha.

Achukue ushauri wa wataalamu wa tasnia yake kama Majani na wengineo aufanyie kazi badala ya kutafuta msuguano usio na tija dhidi ya waliomsaidia kufika alipo leo.

LEAVE A REPLY