AU yashindwa kumpata mrithi wa Dlamini-Zuma

0
148
AU: Viongozi wa juu wa nchi za Afrika kwenye picha ya pamoja jejune Kigali, Rwanda.

Wakuu wa nchi za Afrika pamoja na wawakilishi mbalimbali wa marais wa Afrika waliokosekana kwenye kikao cha AU kilichofanyika leo jijini Kigali nchini Rwanda wameshindwa kumpata mwenyekiti mpya wa Umoja huo kufuatia kutofikiwa kwa zaidi ya nusu ya kura kwa mgombea yeyote.

 

Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa makamu wa zamani wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe alienguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho kwenye mchujo wa awali huku wagombea waliosalia kila mmoja akishindwa kuwashawishi wapiga kura kumpa zaidi ya nusu ya kura zote.

Inadaiwa kuwa wagombea hao walikosa baadhi ya kura za mataifa kutokana na kukosa uzoefu wa kutosha.

Mwenyekiti wa sasa wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma ameendelea kuiongoza AU hadi pale uchaguzi mwingine utakapofanyika. Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa:

Specioza Wandira Kazibwe, na mawaziri wa zamani wa mambo ya nje wa nchi za Botswana, Pelonomi Venson-Moitoi na Equatorial Guinea  Agapito Mba Mokuy.

 

LEAVE A REPLY