AU kupeleka jeshi lake Sudan Kusini

0
89

Wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) wamepitisha mpango wa kupeleka jeshi la Afrika nchini Sudan Kusini ili kusaidia ulinzi na usalama kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.

Jeshi hilo la Afrika linatarajiwa kupewa mamlaka makubwa zaidi ya kiutendaji ikilinganishwa na jeshi la Umoja wa Mataifa (UN) ambalo kwa sasa lipo nchini humo likilinda amani.

Kamishna wa masuala ya usalama wa AU, Smail Chergui amenukuliwa akisema kuwa vikosi vya AU viko tayari kuingia kwenye mapambano na kukabiliana na hali ngumu.

Kamishna Chergui ameongeza kuwa vikosi vya Umoja wa Mataifa havina mamlaka ya kulazimisha amani.

Kikosi cha wanajeshi imara 12,000 cha Umoja wa mataifa kimeshindwa kudhibiti vurugu baina ya vikosi viaminifu kwa rais Salva Kiir na vikosi viaminifu kwa mpinzani wake, makamu wa rais, Riek Machar.

Inasadikiwa kuwa zaidi ya watu 300 wameuawa na wengine maelfu wamebaki bila makazi kufuatia vurugu zilizozuka mwanzoni mwa mwezi huu.

LEAVE A REPLY