Aslay na Nandy wapigwa faini kisi wimbo wa ‘Subakher Mpenzi’

0
457
Wanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay na Nandy wametozzwa faini ya milioni 5 kwa pamoja baada ya kukiri na kukubali kosa kuimba wimbo wa ‘Subalkheri Mpenzi’ bila kufanya mawasiliano na wamiliki wa wimbo huo.
Kikundi hicho kilikusudia kuwafikisha mahakamani wasanii hao lakini kabla ya kuchukua hatua hiyo Aslay na Nandy wakiwakilishwa na kiongozi wao walifika visiwani humo na kufanya mazungumzo na kikundi hicho ambapo wamehitaji kulipwa milioni tano.
Katibu Mkuu wa kikundi cha utamaduni cha tarabu asilia, Taimur Rukuni Twaha, amesema kikundi  hicho cha tarab kimewataka wasanii hao kulipa faini kutokana na kuimba wimbo huo bila ya ridhaa yao.
Twaha amesema licha ya kukiri makosa hayo pia meneja huyo wa Aslay ameomba kuingia mkataba na kikundi hicho cha tarab kufanya biashara ya kuziimba tena nyimbo zao zengine za zamani.
Pia amesema kuhusu nyimbo zao kuimbwa tena hilo bado hawajaafikiana kwa sababu walishapewa agizo na Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour Juma wakati akiwa rais, kuwa wasikubali nyimbo zao za tarabu asilia kuzibadili na kuzifanya katika mfumo wa muziki wa kisasa.

LEAVE A REPLY