Aslay na Nandy wapata mwaliko wa Makamo wa Rais

0
323

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan jana aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni.

Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kujiepusha na makundi mabaya.

Wamamuziki hao walirudia wimbo wa Subakheri ulioimbwa na aliyekuwa mwanamuziki wa Taarab nchini, Nasma Khamis Kidogo.

Kwa upande wa makamo wa Rais amewapongeza wasanii hao kwa wimbo huo ambao kwasasa unafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio nchini.

LEAVE A REPLY