Aslay aweka rekodi Boomplay

0
88

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ametwaa tuzo nne kwa mpigo kutoka kwenye mtandao wa kusambaza muziki ya Boomplay Music baada ya nyimbo zake kufanya vizuri kwenye mtandao huo.

Aslay amekabidhiwa tuzo hizo kufuatia EP yake ya Kipenda Roho kufi kisha zaidi ya wasikilizaji milioni moja ndani ya mtandao huo.

Nyimbo zake mbili za Likizo na Natamba, nazo zimeweka rekodi zake baada ya kufikisha wasikilizaji zaidi ya laki tano na kukabidhiwa tuzo hizo.

Baada ya kutwaa tuzo hizo nne Aslay ameungana na wasanii wenzake kama Nandy, Jux ns Mbosso ambao nao wametwaa tuzo hizo japokuwa yeye anawazidi kwa idadi ndani ya mwaka huu.

Meneja wa msanii huyo Chambuso ambapo alifunguka kuwa, wamefurahishwa mno kuona msanii wao ameweza kuonekana kwenye tuzo hizo na kwamba siyo jambo dogo hivyo wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo.

Aslay ni mmoja wa wasanii wanne waliokuwa wakiunda Yamoto Band ambapo baada ya kusambaratika kwake, kila mmoja alianza kujitafutia malisho kivyake.

LEAVE A REPLY