Aslay amuweka wazi mpenzi wake mpya

0
1212

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ameweka wazi penzi lake zito na Mrembo ambaye ni Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimaro.

Wiki chache zilizopita Aslay alithibitisha kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Tessy Chocolate  ambaye pia ni mama wa mtoto wake mmoja wa kike anayeitwa Moza.

Aslay na Tessy hawa kuweka wazi sababu za kuachana lakini kila mmoja alisisitiza wameachana kwa wema na hawana chuki baina yao.

Aslay amemuanika Rasmi mpenzi wake Mrembo Diana Kimaro kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemposti mara mbili huku akionyesha wazi kuwa wana mahusiano zaidi ya urafiki.

Aslay ameweka wazi suala hilo baada ya kuachana na mpenzi wake Tessy Chocolate aliyezaa bae mtoto mmoja ambaye ni wa kike.

LEAVE A REPLY