Aslay akataa kufananishwa na Alikiba

0
191

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amewataka mashabiki zake kuacha kumlinganisha yeye na mkongwe Alikiba kwa madai bado hajaweza kufika hatua aliyokuwa nayo Kiba.

Aslay ametoa kauli hiyo baada ya kupita kipindi kirefu kwa baadhi ya mashabiki kudai uwezo aliokuwa nao kwa sasa  anaweza hata akamfunika Alikiba pindi wakiamua kufanya ‘show’ ya pamoja au hata wakiandaa tamasha siku moja basi watu wengi wataenda kwa Aslay.

Amesema kuwa “Kama kuna mashabiki wanafanya kitu kama hicho wanakosea kabisa tena sio vizuri, kwa maana hao wameshafika katika level zingine, na mimi ninajitahidi nifike huko siku moja. Kwa hiyo ukinishindanisha kwanza utaniua kisaikolojia kwasababu nitajiona na mimi nimeshafikia hatua zao kumbe bado sana”.

Pamoja na hayo, Aslay ameendelea kwa kusema “ukisema umlinganishe Aslay na Alikiba utakuta kuna vitu vingi vinakukosoa kwsababu yeye ameshaingia katika Tuzo mbalimbali kubwa mpaka kufika sasa hivi na hata akifanya ‘show’ anajaza watu kwa hiyo mimi naona sio watu wa kushindana nao sasa hivi”.

Kwa upande mwingine, Aslay amesema muda huu kwake sio wa kushindana na wasanii waliyomzidi ufanisi na uwezo wa kimuziki bali anajikita zaidi katika kujiboresha ili nae siku afike walipofika wanamuziki wakubwa waliopo nchini Tanzania.

LEAVE A REPLY