Aslay akanusha kutoka kimapenzi na Nandy

0
238

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amekanusha tetesi za kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Nandy.

Kauli hiyo ya Aslay imekuja kufuatia kuenea kwa habari katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao ni wapenzi jambo ambalo mwanamuziki huyo amelipinga vikali sana na kudai kuwa ukaribu wao ni wa kikazi tu.

Aslay amesema kuwa hawezi kutoka kimapenzi na Nandy kwasababu tayari yeye anampenzi wake na anafamilia hivyo ni vigumu kuanzisha mahusiano na mtu mwingine.

Sababu iliyofanya kuzuka kwa taarifa hiyo ni ukaribu uliopo kwasasa kati ya wawili hao mara baada ya kufanya wimbo wa pamoja ‘Subhakher Mpenzi’ pamoja na kufanya show ya pamoja mwezi uliopita.

Kwa upande mwingine Aslay amewataka mashabiki zake kuendelea kumsapoti kwenye kazi zake ili aendelee kufanya kitu kizuri.

LEAVE A REPLY