Aslay akabidhiwa tuzo kutoka Boomplay

0
97

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amekabidhiwa tuzo nne na kampuni ya Boomplay baada ya EP yake kutazamwa na mara milioni 1 kwenye mtandao huo.

Aslay amekabidhiwa tuzo hizo kupitia EP yake ya Kipenda Roho ambayo imefikisha streams zaidi ya milioni 1 katika mtandao huo toka alipoiachia rasmi mapema mwaka huu.

Pia nyimbo kama ‘Natamba, Likizo nazo pia zimepewa tuzo kwa kufikisha watazamaji laki tano kwenye mtandao huo kwa kutazamwa na watu wengi.

Mbali na tuzo hizo pia msanii huyo amekabidhiwa plaque ya steams zote alizofikisha kwenye app ya Boomplay ambayo ni plaque yennye zaidi ya stream milioni tano.

LEAVE A REPLY