Askari wa kike kuwalinda waathirika wa utekaji wa Boko Haram

0
151

Polisi kwenye jimbo la kaskazini-mashariki mwa Nigeria la Borno limeamua kuwapeleka askari wa kike 100 kuwalinda wasichana waliotoroka mikononi mwa kundi la Boko Haram.

Hali hiyo imefuatia ripoti iliyotolewa na shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch inayowatuhumu askari wa kiume kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia wasichana hao ikiwemo kuwabaka.

Askari hao wa kike waliotolewa kutoka maeneo mbalimbali pia wamepewa jukumu la kufanya uchunguzi wa ukweli wa taarifa zilizochapishwa kwenye ripoti hiyo.

Rais wa Nigeria akijibu kuhusiana na ripoti hiyo alikaririwa akisema ‘ameogopeshwa’ na ‘amestushwa’ na ripoti hiyo kuhuyu mambo yaliyokuwa yakiendela kwenye kambi hiyo na kuamuru uchunguzi wa haraka ufanyike.

Ripoti ya HRW inadai kuwa wasichana na wanawake wamekuwa wakilazimishwa kwenye kufanya ngono na wamekuwa wakitelekezwa pindi wanaposhika mimba.

LEAVE A REPLY