Asilimia 64.3 za ‘School Bus’ Dar es Salaam hayana ubora

0
123

Jeshi la usalama Barabarani, Kanda maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa mabasi 119 kati ya 185 ya kubeba wanafunzi yaliyofanyiwa ukaguzi  yamebainika kutokuwa na sifa kutokana na ubovu wa magari hayo.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Awadhi Haji wakati akitoa ufafanuzi juu ya mabasi hayo.

Kamanda Awadhi amesema kuwa hadi juzi walikuwa wamefanya ukaguzi wa magari 185 na 119 kati ya hayo, yamebainika kuwa na makosa mbalimbali.

Amesema kuwa ‘Hadi sasa tumekagua magari 185 kwa Mkoa wa Dar es Salaam 119 tumeyakuta yana upungufu mwingi ikiwamo ubovu wa bodi, matairi chakavu na viti vibovu,”.

Mabasi hayo, maarufu kama ‘school bus’,  ambayo yamebainika kuwa hayana sifa, ni sawa na asilimia 64.3.

Mabasi hayo yanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kubainika kuwa yana makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubovu na uchakavu wa mabasi hayo.

LEAVE A REPLY