Arsenal na United zinamfukuzia ‘Yaya Toure’

0
204

Wakala wa kiungo wa Manchester City na mwanasoka bora wa zamani wa Afrika kwa miaka minne Yaya Toure, Dimitri Seluk amedai kuwa klabu kubwa za Uingereza za Arsenal na Manchester United zinamtaka kiungo huyo.

Toure mwenye miaka 33 na ambaye haonekani kupewa nafasi kwenye kikosi cha kocha wa sasa wa Man City, Pep Guardiola yuko mbioni kusaini mkataba wa awali na klabu mojawapo ya Ulaya mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Wakala wake amedai kuwa licha ya klabu hizo za Uingereza kumtaka nahodha huyo wa Ivory Coast lakini hatosajiunga na klabu yoyote kati ya hizo ingawa pia amekanusha tetesi za mchezaji huyo kwenda kucheza soka la kulipwa nchini China.

Guardiola tayari ameshambashiria Toure kuwa hatakiwa kwenye timu hiyo baada ya kumuacha kwenye kikosi cha mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Wakala huyo pia amedai kuwa klabu ya Manchester City itapoteza mashabiki wengi barani Afrika kutokana na vitendo anavyofanyiwa Toure na kocha wa timu hiyo Guardiola.

Yaya Toure na Guardiola waliwahi kufanya kazi pamoja kwenye klabu ya Barcelona kabla ya Guardiola kumfukuza Toue kwenye kikosi hicho.

Manchester City inatarajia kupambana na mahasimu wao Manchester United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford.

LEAVE A REPLY