Arsenal kumuuza Sanchez mwezi Januari

0
97

Klabu ya Arsenal inazidi kukosa uvumilivu juu ya Alexis Sanchez na inaelezwa kuwa wapo tayari kupokea ofa yoyote isiyopungua paundi milioni 35.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alitolewa ofa ya paundi milioni 60 na Manchester City majira ya joto, lakini Gunners walikataa kwani hawakuweza kupata mbadala wake kwa wakati huo.

Hata hivyo wanaweza kuwa tayari kusikiliza ofa dirisha la uhamisho litakapofunguliwa – lakini kwa bei pungufu.

Wanaamini kwamba moyo wa mchezaji huyo unawaza zaidi kutimkia Man City ya Pep Guardiola.

Lakini kwa sababu atapatikana kama mchezaji huru mwisho wa msimu, mchezaji huyo wa Chile angependelea kubaki hadi aweze kuongeza thamani yake kwa maana ya kiwango.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanakerwa na ulegevu anaouonyesha mchezaji huyo kwa kutofanya juhudi – wakisema ni bora angeondoka majira ya joto.

Inaaminika kuwa Sanchez alikubali mkataba mpya Arsenal – Lakini akabadili mawazo yake.

Paris Saint-Germain wanavutiwa kumsajili mshambuliaji huyo – na pia wanaweza kumtumia Julian Draxler ambaye Arsenal wamekuwa wakimtamani siku nyingi kukamilisha uhamisho huo.

Lakini inaaminika Sanchez alikubali dili jipya miezi 12 iliyopita lakini alibadili akili yake Arsenal walipodhalilishwa na Bayern Munich kwa jumla ya kipigo cha mabao 10-2 Ligi ya Mabingwa kwa mujibu wa The Times.

Sasa kazi ipo kwa Arsenal Januari, wang’ang’anie kubaki na mchezaji asiye na furaha klabuni au wamuuze kwa mahasimu wao wa Ligi Kuu Januari.

 

LEAVE A REPLY