Arnold Schwarzenegger ashambuliwa kwa teke Afrika Kusini

0
495

Kanda ya video imeonyesha kuwa nyota wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger akishambuliwa katika hafla moja nchini Afrika Kusini.

Gavana huyo wa zamani wa jimbo la California mwenye umri wa miaka 71 alikuwa akizungumza na mashabiki wake wakati wa mashindano ya kuruka kamba katika hafla yake ya michezo barani Afrika wakati mtu mmoja alipompiga teke kutoka nyuma.

Mshambuliaji huyo baadaye anaonekana akishikwa na kuzuiliwa baada ya tukio hilo la kumpiga staa huyo.

Hatahivyo Schwarzenegger aliwashukuru mshabiki wake katika mtandao a Twitter wakiotaka kumjulia hali na kusisitia kuwa hakuna cha kujali.

Kanda hiyo ya Video iliosambazwa sana katika mitandao ya kijamii inamuonyesha Schwarzenegger akipiga picha na mashabiki wake katika mji wa Johannesburg katika hafla hiyo ya Jumamosi wakati mtu huyo alipomshambulia kwa teke kutoka nyuma yake.

Nyota huyo wa The Terminator anakaribia kuanguka baada ya teke hilo , huku mshambuliaji wake akianguka chini ambapo anakamatwa na walinzi.

Baadaye Schwarzenegger alituma ujumbe wa Twitter kwa zaidi ya wafuasi wake milioni nne: Nilidhani nilisukumwa na kundi la watu , kitu kinachotokea mara kwa mara . niligundua kwamba nilipigwa teke wakati nilipoona kanda ya video kama mulivyoona.

LEAVE A REPLY