Anna Mghwira wa ACT – Wazalendo kugombea ubunge jimbo la Singida 2020

0
153

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama cha siasa ACT – Wazalendo, Anna Mghwira amesema kuwa atagombea ubunge jimbo la Singida katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Mwanamama huyo ambaye alionyesha ujasiri mkubwa katika mbio za kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

“Siwazi siioni Tanzania ya uchaguzi ya mwaka 2020. Hatuna chaguzi za demokrasia bado. Pengine naweza kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini mwaka 2020,”.

Katika hatua nyingine Mama Anna aliishauri serikali kuwekeza katika kilimo ili kuiandaa Tanzania ya Viwanda.

“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda bila ya kuboresha kilimo kwanza, Tunahitaji kuwa na Tanzania ya kilimo kwanza,”.

LEAVE A REPLY