Anna Mghwira ajiunga CCM akitokea ACT-Wazalendo

0
226

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ametangaza rasmi kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM akitokea ACT-Wazalendo.

Mghwira ametangza hayo leo mjini Dodoma kwenye uzinduzi wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa CCM (UWT), ambao umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika mkutano huo mama Anna Mghwira amesema ameamua kufanya hivyo baada ya kuona jitihada za CCM katika kuleta maendeleo, hivyo akaona ni vyema akajiunga nao.

Mama Anna Mghwira anakuwa kiongozi mkubwa wa tatu kitaifa wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM ndani ya mwaka huu.

LEAVE A REPLY