Angelique Kidjo ashinda tuzo ya Grammy

0
68

Mwanamuziki wa Benin, Angelique Kidjo ameshinda tuzo ya Grammy, Ushindi wake aulekeza kwa Burna boy baada ya kuikosa tuzo hiyo.

Msanii mkongwe, muigizaji na mwandishi kutoka nchini Benin Angelique Kidjo mwenye umri wa miaka (59) ameibuka mshindi wa Tuzo ya Grammy kwenye kipengele cha “Best World Music Album” na kumpiga chini Burna Boy ambaye pia alikuwa anawania kipengele hicho.

Mbali na kushinda tuzo hiyo Angelique Kidjo ameu-dedicate Ushindi wake kwa msanii huyo kutoka nchini Nigeria Burna Boy.

Kwenye hotuba yake ya ushindi alisikika akifunguka kwa kusema kuwa “Hii Tuzo ni Ya Burna Boy, Ni mmoja ya wasanii wadogo ambao wanabadilisha mtazamo wa dunia kuhusiana na Afrika”
.
Ikumbukwe kuwa mwanamama huyo Angelique Kidjo ni mshindi wa mara 4 Tuzo hiyo kubwa kabisa duniani, Aliwahi kushinda tuzo hiyo Mwaka 2008, 2015,2016 na Mwaka huu 2020.

Tuzo hizo zimeingia ukungu usiku wa kuamkia leo kufuatia kifo cha Kobe Bryant. Nyota kibao wameshinda tuzo akiwemo Tyler The Creator ambaye ameshinda tuzo ya album bora ya Rap, IGOR.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Tyler kwenye Grammys, na ameziangusha album za wakali kama; Dreamville (Revenge of the Dreamers III), Meek Mill (Championships), 21 Savage, (i am > i was) na YBN Cordae (The Lost Boy).

 

LEAVE A REPLY