Amini na Linah ndani ya mahaba mazito

0
57

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga na msanii mwenzake Amini wote waliokuwa chini ya THT wameibua Tetesi Za kurudiana Baada ya kuposti picha wakiwa pamoja.

Linah na Amini waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma Lakini walikuja kuachana na Linah alikuwa na mwanaume mwingine ambaye amezaa naye Mtoto mmoja.

Wiki chache zilizopita Linah aliweka wazi kuwa yeye na baba Watoto Wake hawapo pamoja ingawa hakutaja sababu ya kuachana kwao na mara moja tetesi zilianza kusambaa kuwa Linah na Amini wamerudiana.

Tetesi hizo zimepamba moto siku ya jana Baada ya kupostiana wakiwa wameshikana viuno na kukaa katika mkao wa kihasara.

Wawili hao walikuwa mkoa wa Iringa walipokuwa wanafanya shoo na kila mmoja aliposti picha ya mwenzake katika ukurasa wake wa Instagram.

LEAVE A REPLY