Amber Rutty aachiwa huru

0
11

Msanii wa muziki Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 3 za Kitanzania.

Amber aliyesota gerezani kwa miezi kadhaa tangu Septemba 25, mwaka jana, baada ya yeye na mumewe kuhukumiwa kifungo.

Amber Rutty na mumewe ajulikanae kama Said Bakary walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milioni tatu kila mmoja.

Wawili hao walihukumiwa baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha zisizokuwa na maadili.

LEAVE A REPLY