Amber Ruth na mpenzi wake wakosa tena dhamana

0
384

Kesi inayomkabilia msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama Amber Ruth na mpenzi wake Said Bakary imeahirishwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Amber Ruth na mpenzi wake huyo wamekosa tena dhamana kwa mara ya tatu katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mshtakiwa Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwezire kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwezire amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi imeahirisha hadi Desemba 10, 2018.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Amber Rutty na mpenzi wake wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15.

LEAVE A REPLY