Amber Lulu akiri kutumia vipodozi

0
66

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ambar Lulu amekiri kutumia vipodozi maarufu kama mkorogo ili kutengeneza muonekano wake.

Amber Lulu amesema tangu zamani alikuwa anapenda kuwa mweupe kitu kilichopelekea kuamua kutumia gharama kubwa kutengeneza rangi hiyo.

‘’Nikwambie kitu kila mtu anafanya kitu anachokipenda, mimi nimweusi lakini nilikuwa napenda kuwa mweupe. So, nilifanya ninachokipenda pia unajua weupe sio kazi rahisi ni expensive (Gharama) natumia hela’’ amesema Amber Lulu

Muimbaji huyo mwenye ‘makeke’ mengi amesema sio rahisi kutumia mkorogo kama watu wanavyodhani hivyo hashauri watu kufanya hivyo kwasababu nigharama kubwa.
‘’unaweza ukatumia mafuta alafu yasikupende, inabidi ubadirishe kwa mwezi naweza tumia mpaka million 2’’ ameongeza Amber Lulu

Hata hivyo, Tafiti za kitabibu zinaonesha ‘mkorogo’ unamadhara makubwa kwenye ngozi ya binadamu, pia kemikali zinazotumika zinaweza kusababisha maumivu sugu yakichwa yanayoweza kukuweka kwenye hatari yakupata kiharusi.

LEAVE A REPLY