Amber Lulu ajutia kupoteza muda kwa Prezzo

0
202

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amefunguka kuwa anajuta kupoteza muda wake kwa aliyekuwa mpenzi wake Prezoo ambaye ni mwanamuziki kutoka Kenya.

Amber Lulu aliyedumu na Prezzo kwa miezi kadhaa kabla ya kumwagana alisema kuwa, wakati akiwa na jamaa huyo alijishusha mno akiamini watadumu, lakini sasa ameamua kumwaga manyanga moja kwa moja na hataki tena kumsikia.

Mwanamuziki amesema kuwa “Kama ni kuumia, nimeumia sana kwa yule kaka (Prezzo), mwisho wa siku nimegundua nimepoteza muda wangu mwingi sana, kumbe mapenzi hayakuwepo hata kidogo’.

Amber Lulu amesema kuwa anajuta sana kuingia kwenye mapenzi na mwanamuziki huyo kwani alikuwa hana mapenzi naye japokuwa yeye alimpenda sana.

Prezzo na Amber Lulu walikuwa wapenzi kwa miezi kadhaa mwaka jana lakini wameachana baada ya kutoelewana kati ya wawili hao.

LEAVE A REPLY