Aliyetaka kumuua rais Reagan kuachiwa mwezi ujao

0
85
Raia wa Marekani John Hinckley Jr, ambaye alijaribu kumuua ‘bila kukusudia’ rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan akiwa madarakani, ataachiwa kutoka hospitali ya magonjwa ya akili mwezi ujao.
John Hinckley Jr ambaye amekuwa kwenye hospitali hiyo kwa miaka 35 alimshambulia rais Reagan kwa risasi na kumjeruhi pamoja na watu wengine wawili nje ya hoteli ya Washngton mnamo mwezi Machi, 1981.
Bw. Hinckley alikutwa hana hatia kutokana na sababu ya ukichaa lakini akapelekwa kwaajili ya matibabu kwenye hospitali ya Washington.
Tayari mahakama imemruhusu chini ya masharti makali kuishi siku 17 kwenye nyumba ya mama yake iliyopo kwenye jimbo la Virginia.
Moja ya masharti aliyopewa Hinckley na mahakama ni zuio la kuzungumza na vyombo vya habari.
Shambulizi hilo la mwaka 1981 lilimjeruhi kichwani afisa habari wa rais Reagan, James Brady na kupelekea madhara kwenye ubongo yaliyosababisha kutumia kiti cha matairi kwa maisha yake yote hadi alipofariki mwaka 2014.

LEAVE A REPLY