Aliyemuapisha Odinga afukuzwa nchini Kenya

0
119

Aliyemuapisha Raila Odinga, Miguna Miguna amefukuzwa nchini Kenya na kupelekwa nchini Canada, chini ya uangalizi wa serikali.

Taarifa kutoka Kenya ambazo zimethibitishwa na mwanasheria wake zinasma kwamba Miguna aliondolewa nchini kwa ndege ya KLM iliyoondoka na Nairobi, saa 4 usiku.

Tukio hilo limetoka muda mfupi baada ya mahakama ya juu ya nchini humo kuamrisha kufutwa kwa kesi zake zote alizofunguliwa, baada ya waendesha mashtaka na pplisi kushindwa kufika mahakamani, na kumpeleka Miguna.

Kitendo cha Miguna kuwa deported kimelalamikiwa na baadhi ya wanaharakati, wakisema hawamtendei haki, kwani mwanasheria huyo ni raia wa Kenya na mzaliwa wa Kenya.

Ifahamike kwamba Miguna ana uraia wa nchi mbili ikiwemo Canada na Kenya, uraia alioupata wakati akisoma na kufanya kazi kule kama mwanasheria.

Miguna alikamatwa na Polisi Ijumaa ya wiki iliyopita kwa kosa la kumuapisha Raila Odinga kitendo ambacho ni kinyume na sheria, lakini aliachiwa kwa dhamana na kukamatwa tena kabla hajatoka.

LEAVE A REPLY