Alikiba aweka kambi ya wiki mbili nchini Nigeria

0
43

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amewataarifu mashabiki wake kuwa anatarajia kuweka kambi ya wiki mbili nchini Nigeria kwa ajili ya kukamilisha albam yake mpya.

Alikiba anayetamba na wimbo wake Infedele ameweka kambi nchini Nigeria mapema wiki hii ambapo atakaa kwa muda wa wiki mbili ili kukamilisha albam yake mpya.

Alikiba ameweka bayana hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika  maneno yafutayo “Lagos for 2 weeks, Album almost done”.

Album ya Alikiba mpaka sasa haijafahamika itaitwaje na itatoka rasmi mwezi gani japo tetesi zinasema kuwa itatoa mwezi April 2021 na itakuwa na nyimbo si chini ya 20.

LEAVE A REPLY