Alikiba kurejea nchini kesho baada ya kumaliza ziara yake Afrika Kusini

0
422

Mkali wa Bongo Fleva, Alikiba kesho anatarajia kurejea nchini baada ya kumaliza ziara yake ya kimuziki katika miji mitano nchini Afrika Kusini.

Alikiba anatarajia kuwasili kesho majira ya saa nane mchana akiwa pamoja na timu yake akiwemo meneja wake Seven Mosha waliokuwa pamoja katika ziara hiyo ya kimuzikiki nchini Afrika Kuini.

Mwanamuziki huyo atakapowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA) atapokelewa na mashabiki wake uwanjani hapo mpaka kuelekea katika Hoteli ya Double Tree ambapo atapata muda wa kuongea na waaandishi wa habari.

Mbali na kufanya ziara nchini Afrika Kusini pia Kiba alikabidhiwa tuzo yake MTV EMA aliyoshinda mwaka jana na kukabidhiwa tuzo kutoka lebo yake ya Sony kutokana na wimbo wake Aje kufikishwa views milioni 5 kwenye mtandao wa Youtube.

Baada ya kumaliza ziara yake nchini Afrika Kusini, Alikiba anatarajia kukwea pipa na kuelekea nchini Marekani siku ya Jumatano kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki katika baadhi ya miji nchini humo.

LEAVE A REPLY