Alikiba kuigiza tamthilia

0
38

Meneja wa wasanii nchini, Max Rioba amefunguka na kusema kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba atakuwa kwenye tamthilia yake mpya itakayotoka hivi karibuni.

Max Rioba ambaye pia ni producer wa muziki amesema kuwa tayari ameshamwambia msanii huyo vitu vikikaa sawa watafanya mambo makubwa kwenye tamthilia hiyo.

Pia Max amesema kuwa “Natamani kufanya kazi na Alikiba na tayari nimeshazungumza naye tayari kuna mipango ambayo tunaiweka sawa na tutafanya kazi pamoja kuanzia kuandika wimbo, kutoa nyimbo, collabo na awe kwenye tamthilia yangu”

Kwa upande wa msanii Alikiba amesema “Max Rioba ni mtu mwenye ‘vision’ tofauti ndiyo maana namkubali katika hilo, hata kwenye video yangu ya mvumo wa radi alifanya kitu, hivyo wategemee kwamba naweza kufanya naye kazi muda sio mrefu, pia nishafanyaga filamu kipaji hicho kipo na nilianzia shuleni na sanaa tunaishi nayo”.

Meneja Max Rioba tayari ameshafanya kazi na wasanii wakubwa hapa Bongo kama Wema Sepetu, Hamisa Mobetto, Shilole na Young Dee.

LEAVE A REPLY