Alikiba kuachia nyimbo mbili mwisho wa mwaka huu

0
601

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameweka wazi kuwa Desemba 29 mwaka huu ataachia nyimbo zake mbili pamoja na kuzindua kinywaji chake cha Mofaya Energy Drink.

Alikiba amefunguka na kuwatangazia mashabiki wake kuwa ile tarehe aliyokuwa ametangaza kwa ajili ya show yake na mama Yyone Chakachaka ambayo ilikuwa ni December 22 itapelekwa mbele na kufanya Februari mwakani.

Mwanamuziki huyo amewataka mashabiki wake kuwa Desemba 22 atakuwa kwenye tamsha la Fiesta ambalo litafanyika siku hiyo katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.

Akiweka ratiba hiyo katika ukurasa wake, alikiba ansema kuwa kufunga mwaka na king kiba ipo pale pale itakayofanyika december 29 lakini siku ya terhr 22 kutakuwa na grand finale ya tamasha la Fiesta hivyo yeye pia atakuwepo kuwapa mashabiki wake kile wanachostaili.

Hii itakuwa habari njema kwa mashabiki kwa sababu kwanza tamsha hilo lilionekana kukosa matumaini ya kufanyika kwa wakazi wa Dar hasa baada ya  kuhairishwa, lakini pia uwepo wa alikiba katika stage unoageza hamasa ya mashabiki wanaotaka kumuona.

LEAVE A REPLY