Alikiba azidi kuweka rekodi Youtube

0
21

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake baada ya ngoma zake tatu alizoziachia kutoka Album yake mpya ya ‘Only One King’ kuingia trending ya mtandao wa Youtube.

Alikiba ameweka rekodi hiyo baada ya kupita siku 6 tangu alivyoiachia Album hiyo yenye ngoma 16, huku akiwashirikisha wasanii wa nje tu.

Albam hiyo ya Alikiba inaendelea kufanya vizuri kwenye platform tofauti baada ya kutoka wiki iliyopita na kutambulisha kila sehemu.

Alikiba amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kuisapoti albam yake toka alitangaza kuiachi hivi karibuni.

LEAVE A REPLY