Alikiba aweka sababu ya kutopost picha ya Sam wa Ukweli

0
918
Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa Imani ya dini yake hairuhusu kuposti picha za marehemu katika mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo ya Alikiba imekuja baada ya baadhi ya watu kumuhoji kwanini ameshindwa kuposti picha ya marehemu Sam wa Ukweli katika mitandao ya kijamii.

Alikiba ameamua kuweka suala hilo sawa baada ya lawama nyingi kwa wadau mbalimbali wa muziki wakidai Kiba hana ushirikiano na wenzake hata katika masuala ya msiba huwa a-post picha ya marehemu na mambo mengine.

Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema “kusema ukweli nimeguswa na kifo cha msanii mwenzetu Sam wa Ukweli. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina Sinza alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

LEAVE A REPLY