Alikiba ataka wasanii watengeneze documentary ya Nyerere

0
15

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amemuomba Dkt. Magufuli atenge bajeti ya fedha zitakazotumika kutengeneza ‘documentary’ ya maisha ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Amesema ikitengenezwa itakuwa na faida mbili, ikiwemo kufanya Nyerere azidi kukumbukwa na kufahamika kwa vijana ambao wamezaliwa baada ya kifo chake.

Pia, amesema itasaidia kuwainua wasanii wa maigizo ambao wamekuwa wakishirikiana nao kwenye majukumu mbalimbali ya kujenga Taifa.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni Rais wa kwanza wa Tanzania, muasisi wa Taifa na mpigania Uhuru aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999.

LEAVE A REPLY