Alikiba asikitishwa na hali ya Chid Benz

0
68

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa anasikitishwa na hali aliyekuwanayo Chid  Benz baada ya kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya kuona mateso anayopitia Chid Benz toka ajiingize kwenye matumizi hayo ya madawa ya kulevya.

Alikiba amsema kuwa anajisikia vibaya kila anapomuona Chid Benz katika hali yake aliyonayo sasa kutokana na utumiaji wa madaya ya kulevya ambao umeharibu sana muelekeo wa maisha yake toka aanze kutumia.

Pia msanii huyo amesema kuwa amekuwa akishangaa na kuumia sana kila anpokumbuka jinsi Chid Benzi alivyokuwa kinara katka muziki lakini tangu alipojiingiza katika madawa imekuwa kama sumu ambayo kila mtu amejitaidi kuiondoa lakini kila anaejaribu anakwama.

Chid Benz amekuwa akisaidiwa na baadhi ya watu ili kuweza kuachana na madawa ya kulevya lakini inashidikana kutokana na kuwa bado moyo wake haujakubaliana na mateso anayoyapata.

LEAVE A REPLY