Alikiba amtimua kazi meneja wake

0
67

Mwaamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amethibitisha kumtimua kazi aliyekuwa meneja wake Esilovey ambaye alikuwa anasimami kazi zake muziki baada ya kuachana na Seven Mosha.

Alikiba amesema kuwa “‘Ni kweli sifanyi nae kazi tena. Ni taratibu za kazi, amekuwa na mchango kwenye kampuni yetu katika kipindi cha nyuma, lakini kuna vitu vilitokea and some misunderstanding na management tukakubaliana tumuondoe.

Lakini sio kwamba hawezi kazi, hapana, ni mchapakazi lakini alienda kinyume kidogo na kazi vilitufanya sisi kumuondoa.

Kuhusu kwamba hili litaleta shida kwenye kampuni hasa baada ya hivi karibuni kuacha kufanya kazi na Seven na sasa Esilovey, Alikiba akajibu: “ Hapana, haitoleta taabu hata kidogo, Esi alikuwa mtu ambaye alikuwa anapenda kufanya hiyo kazi.

Alikiba amesema kuwa baada ya kuondoka kwa meneja huyo kila kitu kipo sawa, ndio maana hatujaona haja kuongeza mtu mwingine.”

LEAVE A REPLY