Alikiba akanusha taarifa za kuacha muziki

0
11

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kukanusha kuacha muziki baada ya taarifa za kuacha muziki kusambaa katika mitandao ya kijamii.

 

Taarifa za mwanamuziki huyo kuacha muziki zilizuka wiki chache zilizopita na kusababisha baadhi ya wapenzi na mashabiki wa mwanamuziki huyo kuanza kuhoji sababu ya mwanamuziki huyo kuacha muziki.

 

Alikiba ameweka wazi kuwa, si kweli kwamba anatarajia kuacha muziki kwani taarifa hizo hazina ukweli kabisa hivyo mashabiki wake waendelee kupata kazi mpya kutoka kwa mwanamuziki huyo.

 

Kiba ameendelea kusema kuwa madai hayo yalikuwa stori za mitandaoni hivyo mashabiki wake watambue kuwa si habari za kweli.

 

Uvumi wa Kiba kuacha muziki umeshika kasi ikiwa ni miezi michache imepita tangu msanii mwingine nguli katika uwanja wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee atangaze kuacha muziki.

 

Pia Alikiba amekanusha kuacha na mkewe Amina Khaleef baada ya habari za wawili hao kuachana kuenea katika mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY