Alikiba aingiza sokoni Mofaya

0
115

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amethibitisha kuingiza sokoni kinywaji chake cha Mofaya ambapo kitaanza kupatikana jijini Dar Es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kiba amefunguka na kutaja maeneo ambayo kitakuwa kinapatikana huku akiwaambia watu wa mikoani wakae mkao wa kula maana kinywaji hicho kitasambaa nchini Nzima.

Kupiatia akaunti yake ya Instagram ameandika “Sasa Mofaya Energy Drink zimeanza kupatikana jijini Dar es Salaam kwa Mawakala Wakuu (main Distributors).

Msanii huyo amesema kuwa baada ya kinywaji hicho kuanza kupatikana jijini Dar es Salaam pia kitaanza kusambazwa katika mikoa yote nchini Tanzania.

Baada ya kuzindua kinywaji hicho msanii huyo anaungana na baadhi ya wasanii ambao pia wameingiza sokoni bidhaa zao kama vile Diamond kupitia Diamond Karanga, Mwana FA ambae ameingiza sokoni bidhaa za pafyum.

LEAVE A REPLY