Alikiba afuta video yake mpya kwenye mtandao wa youtube

0
214

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameamua kufuta video ya wimbo wake mpya kwenye mtandao wa youtube masaa kadhaa baada ya kuachia hewani.

Alikiba aliachia kazi hiyo usiku wa kuamkia Jumatano hii baada ya kukaa muda mrefu bila kuachia kazi hali ambayo iliwafanya mashabiki wake wachukizwe na kitendo hicho.

Hata hivyo baada ya kuachia wimbo huo, mashabiki walionekana kutoridhishwa na kazi hiyo huku wengine wakidai kwamba wimbo huo ameuridia wimbo wake wa zamani.

Baada ya kuupachika wimbo mtandaoni, mashabiki walionekana kuuponda kwa madai amerudia wimbo wake wa zamani.

Huenda komenti hizo ndio nimemfanya muimbaji huyo kuondoa video hiyo YouTube kwani komenti nyingi zilikuwa zinamponda kutokana na kuchelewa kuachia nyimbo.

LEAVE A REPLY