Alikiba afunguka suala la uvaaji wake

0
26

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa kwasasa hawezi kuvaa hereni au kusuka nywele kwasababu fashion hiyo ishapita na wakati kwa upande wake.

Alikiba amesema suala la uvaaji kwenye video zake halimsumbui tena maana mambo mengi ameshayapitia kwenye muziki wake na kusema kuwa kwa sasa anaangalia ubunifu mwingine.

”Mambo ya kuvaa sijui hereni masikioni na vitu vingine vya aina hiyo, nadhani kwangu muda wake ulishapita.

Pia amesema kuwa Hata mitindo yangu ya sasa kuanzia uvaaji wangu kwenye video nadhani unafaa kwasababu watu wanaohusika na ubunifu wanafanya kazi yao,” amesema Alikiba.

Katika hatua nyingine Alikiba amesema moja ya sababu kubwa ya kuimba kwa lugha ya kifaransa kwenye ngoma yake mpya Infidele ni kutokana na lugha hiyo kutumiwa na watu wengine duniani hivyo kuna uwezekano wa muziki wake kuwafikia watu wengi.

LEAVE A REPLY